Musa Mwafrika, maarufu pia kama Musa Mwizi (330–405), alikuwa mmonaki
padri nchini Misri na mmojawapo kati ya mababu wa jangwani.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Julai na tarehe 28 Agosti.
Mzaliwa wa Ethiopia, Musa alikuwa mtumishi wa afisa wa serikali nchini Misri mpaka alipofukuzwa kwa thuhuma za kuiba na kuua.
Akiwa jitu, akawa bosi wa kundi la majambazi lililotisha watu wa bonde la Nile kwa ukatili.
Alipojaribu kukwepa waliokuwa wanamwinda, alifichama kwa wamonaki wa
jangwani huko Wadi El Natrun (Sketes), karibu na Alexandria. Juhudi za
kiroho, utulivu na furaha walivyokuwa navyo vilimuathiri kwa dhati. Muda
mfupi baadaye aliacha mtindo wake wa kuishi, akabatizwa na kujiunga na
monasteri ile.
Kwanza alipata shida sana kuzoea nidhamu ya jumuia ile. Alipovamiwa na wezi chumbani
mwake, aliwazidi nguvu akawaburuza hadi katika kikanisa walimokuwemo
wenzake wakisali ili aambiwe awafanyie nini wageni hao.
Musa alikuwa na ari katika yote aliyoyafanya, lakini alikata tamaa
alipojitambua si mkamilifu kutosha. Hapo abati Isidori alimchukua
alfajiri hadi juu ya paa ili kutazama miali ya kwanza ya jua. Halafu
akamuambia, “Taratibu tu miali ya jua inaondoa usiku na kuleta mchana
mpya, na vilevile taratibu tu mtu anakuwa mwanasala kamili.”
Baadaye Musa akawa mwenyewe kiongozi wa jumuia ya wakaapweke katika sehemu nyingine ya jangwa akapewa upadrisho.
Alipokuwa na umri wa miaka 75 hivi, ilisikika kwamba kundi la
Waberber limepanga kushambulia monasteri yao. Wenzake walitaka kujihami,
lakini Musa aliwazuia akawaambia ni afadhali wakimbie kuliko kushika
silaha. Mwenyewe na wengine 7 walibaki hadi walipouawa tarehe 1 Julai.
Kwa sababu hiyo Musa Mwafrika anaheshimiwa leo kama mtetezi wa msimamo wa kukataa silaha katika kudai haki.
Source: Wikipedia
Icon of st Moses the Ethiopian
Ona pia
Moses the Ethiopian, the Black Saint & Teacher (& other Ethiopian saints in the Orthodox Church)
St MOÏSE L'ÉTHIOPIEN (ou "Le Noir" ou "Le Fort") et... Shawn "Thunder" Wallace
Brotherhood of St. Moses the Black
Watakatifu
Wakristo Orthodox ya Afrika
Ancient Christian faith (Orthodox Church) in Africa
The Orthodox Church of Alexandria & the Patriarchate of Alexandria
The holy anarchists... in the Egyptian Desert
"Oriental Orthodox"
St Moses the Ethiopian,
Greek Orthodox holy icon