Africa of my heart
Mtakatifu
Martino wa Tours (Savaria, Panonia, leo Hungaria 316 –
Candes-Saint-Martin, Gaul, leo Ufaransa 397) alikuwa mmonaki, halafu
askofu (kuanzia 371 hadi kifo chake).
Alipokaribia kifo, walimuomba asiondoke,
naye akasali hivi: “Ee Bwana, nikihitajiwa bado na watu wako, sikatai
uchovu wa kazi: utakalo lifanyike!”
Maisha yake yaliandikwa na Sulpicius Severus yakawa kielelezo cha vitabu juu ya watakatifu.
Sifa yake ilienea haraka hivi kwamba aliheshimiwa kama mtakatifu ingawa hakuwa mfiadini kama kawaida ya wakati ule.
Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 8 Novemba.
Ona pia
Bikira Maria, Mama wa Mungu
Yesu Kristo: "Ninyi ni nuru ya ulimwengu"!...
Vijito Vya Maji Yaletayo Uzima - "Mtu ye yote mwenye kiu na aje kwangu anywe"
Kanisa la Orthodox
Δεν υπάρχουν σχόλια:
Δημοσίευση σχολίου