Παρασκευή 30 Οκτωβρίου 2015

Ulaji wa nyama za binadamu na jinai nyingine S/Kusini


Iran Swahili Radio

 Ulaji wa nyama za binadamu na jinai nyingine S/Kusini Ripoti iliyotolewa hivi karibuni imefichua kuwepo vitendo vya kuwalazimisha watu kula nyama au viungo vya ndani ya miili ya wanadamu wenzao, kunywa damu, ubakaji na vitendo vingine vya ukatili kutoka pande zote mbili zinazohusika katika mzozo  huko Sudan Kusini.
Ripoti hiyo ni matokeo ya uchunguzi uliofanywa na Kamisheni ya Uchunguzi ya Umoja wa Afrika kuhusu Sudan Kusini. Ripoti hiyo imeituhumu serikali na waasi wa Sudan Kusini kuwa wamefanya ukatili na unyanyasaji mkubwa kwa raia wa nchi hiyo. Ripoti hiyo yenye kurasa 342 imeongeza kuwa, kuna ushahidi wa kutosha kwamba mauaji, vitendo vya ubakaji, utumwa wa ngono, mateso na aina nyingine za ukiukaji wa haki za binadamu vimefanywa na pande mbili husika kwenye mzozo wa Sudan Kusini. Madai ya kutolewa damu kutoka katika miili ya watu mara baada ya kuuliwa na kuwalazimisha wengine kutoka kabila mojawapo la jamii ya nchi hiyo kunywa damu au kula nyama zilizochomwa za miili ya wanadamu wenzao, ni miongoni mwa jinai zilizoorodheshwa katika ripoti hiyo ya AU.

Ona pia

«I lit the charcoal briquettes at the one end of a magazine of bullets from a kalashnikov, placed the incense on top of them and censed the people accompanying me» (Experiences from South Sudan)

Δεν υπάρχουν σχόλια:

Δημοσίευση σχολίου