Δευτέρα 12 Οκτωβρίου 2015

Malengo ya Milenia kuhusu baa la njaa


IDHAA YA KISWAHILI

Katika kikao cha viongozi wa nchi duniani mwaka wa 1996 kuhusu chakula, waliohudhuria ikiwamo jamii ya kimataifa, waliahidi kupunguza kwa nusu idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani. 


Miaka mitano baadaye, Malengo ya Milenia yalichangia kupunguza kiwango hicho kwa kulenga tu kupunguza kwa nusu idadi ya wanaokabiliwa na baa la njaa. Ripoti ya hivi karibuni kuhusu utoshelezo wa chakula ya mwaka wa 2015 iliyotolewa na Shirika la Chakula la Kilimo Lenye makao yake mjini Rome, shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP na Mfuko wa Dunia kuhusu Kilimo na Maendeleo, inakadiriwa kuwa watu takribani milioni 795, au mmoja miongoni mwa watu tisa kote duniani wanaendelea kukabiliwa na baa kubwa la njaa.
Idadi ya wanaokabiliwa na kiwango cha kukithiri cha utapiam lo kote duniani imepungua kwa kiasi kinachozidi kwa kiwango kidogo, moja kwa tano kutoka watu milioni 1010.6 mwaka wa 1991 hadi milioni 929.6 mwaka wa 2001, milioni 820.7 mwaka wa 2011 na milioni 794 mwaka wa 2014.
Kutokana na kupungua kwa idadi ya wanaokumbwa na baa kubwa la njaa katika mataifa yanayoendelea kutoka milioni 990.7 mwaka wa 1991 hadi milioni 779.9 mwaka wa 2014, mgao wao katika mataifa hayo umepungua kwa asilimia 44.4, kutoka asilimia 23.4 hadi 12.9 katika kipindi cha miaka 23 iliyopita, lakini ungalipo upungufu wa asilimia 11.7 wa malengo yaliyowekwa.
Hivyo basi, lengo la kupunguza kwa nusu idadi ya wanaokabiliwa na baa kubwa la njaa duniani ifikiapo mwaka wa 2015 huenda lisitimizwe kutokana na juhudi zilizowekwa. Hata hivyo ungalipo uwezekano wa kutimizwa kwa lengo hilo, kupitia juhudi zaidi na za haraka kuchapusha mchakato huo, hasa katika nchi ambazo hazijapiga hatua zilizotazamiwa kufikia sasa.


Ikumbukwe kuwa idadi kubwa ya wanaokabiliwa na baa la njaa wako katika mataifa yanayoendelea. Baadhi ya mataifa yanajikokota katika kutokomeza baa la njaa, huku idadi ya wanaoathiriwa ikiongezeka.Kufikia mwishoni mwa mwaka wa 2014, mataifa 72 miongoni mwa 129 yanayoendelea yaliyofanyiwa uchunguzi yametimiza malengo ya milenia kwa ama kupunguza kwa nusu idadi ya wanaokabiliwa na baa la njaa au kupungaza idadi hiyo hadi chini ya asilimia 5. Mataifa mengine vilevile yanatarajiwa kufanya hivyo ifikiapo mwaka wa 2015.
Badala ya kupunguza idadi ya wanaokabiliwa na baa la njaa katika mataifa yanayoendelea kwa kiwango cha watu milioni 476, idadi hii ilipunguzwa tu kwa kiwango cha watu milioni 221, chini ya nusu ya idadi ya awali.
Hata hivyo, mataifa 29 yalifanikiwa kupunguza kwa nusu idadi ya wanaokabiliwa na njaa. Hatua hii ni muhimu kwa vile inaonesha kuwa kuafikia na kupiga hatua ya kupunguza baa la njaa, ni halisi.
Tofauti zilizopo hukusu utapiamlo uliokithiri unashuhudiwa katika maeneo yote. Aidha upo upungufu ulio wazi kuhusu mweneo na idadi hiyo katika mataifa mengi Kusini Mashariki ya Asia, Asia Mashariki, Asia ya Kati, Kusini mwa Marekani na Caribbean ambako malengo ya milenia ya kupunguza baa la njaa kwa nusu yametimizwa.
Huku mataifa yaliyo kusini mwa jangwa la sahara yakiwa na idadi kubwa ya wanaokabiliwa na baa la njaa, takribani mmoja miongoni mwa watu wanne, Kusini mwa Asia kuna idadi kubwa zaidi, ambako takribani watoto nusu bilioni wanakabiliwa na utapiamlo. Kusini mwa Asia pekee limeshuhudiwa ongezeko la watu wanaokabiliwa na njaa ikilinganishwa na mwaka wa 1991, huku hatua katika mataifa ya Kusini mwa jangwa na sahara, Asia Kusini ikiwa haijapigwa katika kutokomeza baa la njaa ifikiapo mwaka wa 2015 kwa mujibu wa malengo ya milenia.
Licha ya mapungufu katika kutimiza malengo ya milenia na kukosa kukaribia lengo lililowekwa kwenye kikao cha viongozi wa nchi la kupunguza kwa nusu idadi ya wanaokabiliwa na baa la njaa, viongozi wa dunia huenda wakaafikiana kuhusu lengo la kupunguza umaskini ifikiapo mwaka wa 2030, kuambatana na tangazo kuhusu maendeleo endelevu katika Umoja wa Mataifa mwezi Septemba.
Kwa hakika, vipo vyakula vya kutosha kuwalisha watu wote duniani. Hata hivyo mamia ya maelfu ya watu hawana njia ya kupata chakula likiwa hitaji la msingi, achia mbali hitali na viinilishe.Kutokana na viwango vya juu vya unyang'ng'anyi na ukosefu wa ajira, huenda hali ya umaskini na njaa isikabiliwe ifikiapo mwaka wa 2030 iwapo kila mtu hatajengewa msingi dhabiti.
Kikao cha pili cha kimataifa kuhusu viinilishe mjini Rome Novemba iliyopita, kiliangazia uwajibikaji na mapendekezo ya kuchapusha mchakato wa kutokomeza uhaba wa viinilishe. Kuboresha hali ya viinilishe kutahitaji mwendelezo wa juhudi za pamoja kuanzia sera faafu, uboreshaji wa hali ya afya, chakula, masuala ya jamii, usafi, usambazaji wa maji na elimu.

Mwandishi: Geoffrey Mung'ou
Mhariri: Saum Yusuf
  • Tarehe 29.05.2015

Δεν υπάρχουν σχόλια:

Δημοσίευση σχολίου