Yohana 7:37-52
Orthodox Metropolis of Zambia and Malawi
Siku ya mwisho ya sikukuu, ambayo kwa kawaida ndio ili kuwa kilele cha sherehe, Yesu alisimama akasema kwa sauti kuu, “Mtu ye yote mwenye kiu na aje kwangu anywe. Kama Maandiko yasemavyo, ye yote aniaminiye, vijito vya maji yaletayo uzima vitatiririka kutoka moyoni mwake.” Yesu alisema haya kuhusu Roho Mtakatifu ambaye wote waliomwamini Yesu wangempokea, kwani mpaka wakati huo, Roho alikuwa bado hajatolewa, kwa kuwa Yesu alikuwa bado hajainuliwa na kutukuzwa.Waliposikia maneno hayo, baadhi ya watu walisema, “Hakika huyu ndiye yule Nabii.” Wengine wakasema, “Huyu ni Masihi!” Lakini wengine wakauliza, “Kwani Masihi kwao ni Gali laya? Je, Maandiko hayakusema kuwa Masihi atakuwa mzao wa Daudi na kwamba atazaliwa Bethlehemu, mji alioishi Daudi?” Kwa hiyo kukawa na mgawanyiko kati ya watu kumhusu Yesu. Baadhi yao walitaka kumkamata, lakini hakuna aliyethubutu kumgusa.
Kutokuamini Kwa Viongozi Wa Wayahudi
Hatimaye wale walinzi wa Hekalu waliokuwa wametumwa kum kamata Yesu, walirudi kwa makuhani wakuu na Mafarisayo. Wakauli zwa, “Mbona hamkumleta ?”
Wale walinzi wakajibu, “Hakuna mtu ambaye amewahi kufundisha kama yeye.” Mafarisayo wakajibu, “Ameweza kuwa danganya hata ninyi? Je, mmewahi kuona kiongozi ye yote au mmoja wa Mafarisayo ambaye amemwamini? Lakini huu umati wa watu wasiojua sheria ya Musa, wamelaaniwa.”
Ndipo Nikodemo, yule aliyemwendea Yesu siku moja, ambaye alikuwa kati yao akauliza, “Je, sheria zetu zinaturuhusu kumhukumu mtu kabla ya kumsikiliza na kufahamu alilotenda?”
Wakamjibu, “Je, wewe pia unatoka Galilaya? Chunguza Maandiko nawe utaona kwamba hakuna nabii anayetokea Galilaya!”
Yohana 8:12
Yesu Ni Nuru Ya Ulimwengu
Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu ye yote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru yenye kuleta uzima.”
Ona pia
Utatu Mtakatifu, Mungu ambaye anapenda ubinadamu
Yesu Kristo - Mungu akawa mtu na mtu inakuwa kama mungu
Bikira Maria, Mama wa Mungu
African Pentecost 2017
Kanisa la Orthodox Watakatifu
Wakristo Orthodox ya Afrika
Kanisa la Orthodox nchini Kenya: Liturujia takatifu, watoto na zaburi - Orthodox Church in Kenya: the holy liturgy, children and psalms
Kristo amefufuka kutoka Kanisa la Orthodox la Uganda / UKrestu yena kunje / Kristu uvukile yobuOthodoki of Uganda / Christ is Risen from Uganda!
Δεν υπάρχουν σχόλια:
Δημοσίευση σχολίου